VAZI HILI LA DIAMOND LASABABISHA VIDEO YA MSANII DULLY SYKES KUFUNGIWA
jana
Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa kwa video yake ya kabinti
special na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu mbili
zilizosababisha video hii kufungiwa na ya kwanza ni kitendo cha msanii
Diamond Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno ambalo ni tusi . Hii
ingekua kwa nchi za mbele basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu
kinaitwa “blurring” yaani wanayafanya maneno yasisomeke lakini wabongo
wakaona isiwe tabu na director akaamua kuacha video irushwe ikiwa katika
hali hii.
Sababu ya pili ni vazi la ufukwe yule demu alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua mbaya.
Je, Unadhani ni haki video hii kufungiwa na kama ni haki je unafikiri ifungiwe ni kwasababu ipi ya msingi?
Source: MWEUSICLASSIC.COM
No comments:
Post a Comment