HAWA NDIO WANACHAMA WA FREEMASON TANZANIA...!HABARI KAMILI HAPA.....
Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600
wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na
watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba
miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.

Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya 600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.
Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.
Chande alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito
wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata
Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi
hilo.
Akizungumzia masharti ya kujiunga
na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini
katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.
Alisema pia ni lazima anayetaka
kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo
hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na
wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.
No comments:
Post a Comment